desktop logo

EXPLORE

DATA

twitterfacebook
mobile logo
news
Tatizo la Ukosefu wa Maji Jijini Nairobi
June 2023
PesaYetu
article

Share

By Erick Mwangi

Maji yana manufaa mengi kwa maisha ya binadamu yeyote kuanzia kwa afya ya mwilini, mazingira na matumizi ya hapa na pale. Ukosefu na uhaba wa maji huleta madhara si haba kama magonjwa mbalimbali miongoni mwao kipindupindu.

Kwa miaka mingi, ukosefu wa maji ukumba  jiji la Nairobi na viunga vyake. Kukabiliana na uhaba huu, serikali ya kaunti imeweka mifumo kadhaa kama mgao unaolenga mitaa kadhaa. 

Kwa mfano, mtaa wa mabanda wa Kariobangi uliopo kata ndogo ya Ruaraka, wakaazi wa eneo hili hupokea maji siku mbili tu kwa wiki nzima.

Kukabiliana na hali, baadhi ya wenyewe wameekeza katika vifaa vya kuhifadhi maji kama njia moja ya kukabiliana na uhaba. 

Kwa upande mwingine baadhi ya wakaazi wanalalama kuhusu uhaba huo wa maji kwani wengi hawana uwezo wa kujikimu kimahitaji  ikizingatiwa kuwa mtungi mmoja wa lita ishirini inauzwa shilingi tano, hivi tatizo la kununua maji ni gharama kivyake katika maisha ya badhi yao. Hata hivyo wametoa wito kwa wahusika kutafuta suluhu ya kudumu.

Juhudi zetu za kuzungumza na usimamizi wa kampuni ya maji ya Nairobi hazikufua dafu hivyo basi tukazungumza na shirika la Inuka Kenya ni Sisi ambalo linashughulikia maswala ya maendeleo ya kaunti pasi na maswala ya maji Nairobi. 

Jacinta Wanjiku ambaye ni mratibu kutoka shirika hilo amesema kuwa ni jukumu la kampuni ya maji ya Nairobi kuhakikisha kwamba wakaazi wa maeneo yote katika kaunti wanapata maji kwa usawa. Kwa upande mwingine ametaja sababu kuu zinazoathiri usambazaji wa maji katika mtaa wa Kariobangi na maeneo mengine katika kaunti ya nairobi.

Huku kaunti ya Nairobi ikikumbwa na uhaba wa maji, washikadau wameweka mikakati kadhaa kuhakikisha wakaazi wanapata bidhaa hii muhimu. Kwa mfano, usimamizi wa jiji chini ya Nairobi Metropolitan Services umefanikisha uchimbaji wa mabawa 193 ya kusambaza maji. Mabawa haya yamechibwa katika kata ndogo zote 17. 

Vile vile ripoti ya CDIP, inaonyesha kuwa ukosefu wa usawa katika mgao wa maji umepelekea wakazi tugemea maji kutoka vituo mbali mabli. 

.frame { position: absolute; top: 0; left: 0; width: 100%; height: 100%; border: 0; z-index: 10; } .wrapper-47-859 { position: relative; overflow: hidden; padding-top: 56.25%; } @media (max-width: 1280px) { .wrapper-47-859{ padding-top: 75%; } @media (max-width: 620px) { .wrapper-47-859 { padding-top: 100%; } @media (max-width: 500px) { .wrapper-47-859 { padding-top: 140%; } }

Kwingineko, kuhakikisha uuzaji wa maji ni wa haki, NMS vile vile inatumia teknolojia kama njia moja ya kuleta uwazi katika sekta hii. 

Image: Kituo cha kuuza maji Nairobi. Source: BBC

Makala haya yameandaliwa na Koch FM, ikishirikiana na Code for Africa, Kenya Community Media Network na baraza la vyombo vya habari katoliki kwa msaada kutoka ushirikiano na Ujerumani kama mradi wa kaunti yetu, jukumu letu.

Related Stories
Usambazaji wa Umeme Jijini Nairobi
By Sharon Gitonga Mkakati wa kuunganisha umeme ni swala ambalo lilipewa kipaumbele pindi tu serikali ya Jubilee ilipojinyakulia uongozi mnamo mwaka wa 2013. Mradi huu umeshuhudiwa kupanuka kwa kasi katika mji wa Nairobi. Sababu kuu  ni kumwezesha mwanachi wa kawaida kujimudu kimaisha. Kulingana na ripoti la CDIP,  jijini Nairobi, takribani asilimia tisini na tano ya […]
logo
This site is a project of Code for Africa, the continent’s largest network of civic technology and data journalism labs. All content is released under a Creative Commons attribution Licence 4.0. Reuse it to help empower your own community.

2022 PesaYetu

Resources
  • About
  • Privacy Policy
  • Terms of Service
Stay in touch with us
instagramfacebooktwitterlinkedin